Uhasibu ni sehemu kubwa ya juhudi yoyote ya biashara na si rahisi kama kujumlisha na kutoa. Wafanyabiashara wadogo wadogo mara nyingi hufikiria utunzaji wa mahesabu yao wenyewe ili kuokoa fedha-lakini hii inaweza kuwa ni wazo bora . Makosa ya kiuhasibu yanaweza kuigharimu kampuni kwa kiwango kikubwa. Hutakiwi kukurupuka, kwa sababu inaweza kuzuia ukuaji wa biashara yako. Wamiliki wa biashara ndogo mara nyingi hufanya makosa katika miaka yao mapema kutokana na ukosefu wa taratibu sahihi za uhasibu.
Haya hapa ni makosa sita ambayo mmiliki wa biashara ndogo lazima ajaribu kuyaepuka;
- Kujaribu kusimamia kila kitu peke yako;
Wajasiriamali, huwa na shauku ya biashara zao, mala nyingi huwa na tabia kutaka kufanya kila kitu wao wenyewe. Ulipoanza, unaweze kusimamia kila kitu mwenyewe. Tatizo hutokea wakati unapojaribu kusimamia maswala ya uhasibu peke yako, unaweza kujikuta ubora wa huduma unazozitoa zinazorota.
Kudumisha akaunti ni muhimu sana kwa biashara yako kwani huisaidia kukua, lakini kazi inayotakiwa ni kutekeleza masuala ya kiuhasibu.
NB. Huwezi kushughulikia kila kitu peke yako, unatakiwa kujifunza jinsi ya kugawa baadhi ya majukumu yako kwa wengine.
Kama mmiliki wa biashara, muda wako ni muhimu, na biashara yako inahitaji mawazo yako ili kukua. Ni mantiki ya kuajiri Muhasibu au mtaalamu kushughulikia akaunti zote za biashara yako.
2. Kutokujua tofauti kati ya mtiririko wa fedha na faida. (cash flow and profit)
Mtiririko wa fedha ni pesa inayoingia na kutoka nje ya kampuni kutokana na shughuli za fedha, uwekezaji na shughuli nyingine.
Faida, kwa upande mwingine, ni kile kinachobaki kutoka mapato ya mauzo baada ya gharama za kampuni hiyo nikutolewa. Hebu angalia mfano: Tuseme umenunua bidhaa kwa 10,000/= na kuuza kwa 20,000/=. Hapa umepata faida ya Tsh.10,000/=. Lakini, Itakuaje kama mnunuzi hawezi kutoa fedha kwa wakati? Katika hali hii, biashara yako itaonyesha faida lakini vipi kuhusu bili unayohitaji kulipa kwa wakati huo huo? Unaweza usiwe na fedha pamoja na faida. hivyo ni vema kujua tofauti ya mtiriliko wa fedha.
kwa kutojua tutofautisha unaweza ukajikuta unarudia makosa hayo ya mara kwa mara , huenda hata kufilisika.
3. Kuchanganya fedha binafsi na fedha za Biashara
Hii ni njia ya haraka na rahisi kuharibu fedha ya biashara yako. Hatua ya kwanza unapofungua biashara ni kufungua akaunti ya benki mara moja ambayo itahusiana na maswala Biashara tu. Inashauriwa kuendesha mapato na matumizi kwa njia ya akaunti ya benki.
unaweza ukawa unaendelea matumizi mengine kutoka mfukoni kwako hata hivyo kuweka rekodi kwa gharama hizo ni muhimu, gharama hizo ni kama makato ya kodi. Kama hakuna rekodi hutaweza kuzitoa hivyo kukusababishia kupoteza hela ambazo ulisahau kuzitunzia kumbukumbu.
ZINGATIA: Tenganisha akaunti yako binafsi na akaunti ya biashara ili iwe rahisi kutambua mwenyendo wa biashara yako.
4. Kutomia programu au teknolojia
Kwa kutumia programu, Utunzaji au uwekaji wa vitabu vyako wa kihasibu kama mishahara na bajeti hufanyika moja kwa moja. Hii huongeza ufanisi, na kukuruhusu kutumia muda wako wa thamani sana kufanya mambo yako mengine.
wahasibu wengi na huamini kuwa Microsoft Excel inaweza kufanya kazi zote za kihasibu kwa ufanisi kama inavyotakiwa. Hata hivyo, ni vizuri kujua kuwa Excel haina kiwango cha juu sana kuifanya kazi isiwe na makosa.
Kwa mfano, hakuna njia inayoweza kutumika kutambua makosa ya kibinadamu inaweza kuchunguzwa katika Excel. Hata hivyo, programu za kihasibu hutumia njia double - entry ambayo inasaidia kugundua makosa ambayo ni vigumu kuyatambua ukiwa unatumia EXcel.
ZINGATIA: Ni vema tukajitaidi kutumia programu za kihasibu ambazo zitaturahisishia kufanya kazi zetu na hata kuokoa muda wetu ambao ni mali.
5. Kutumia mbinu zenye unafuu
Hili nalo pia limekua ni tatizo kwa wafanya biashara wadogo wadogo, huamua kutafuta mbinu ambazo wanadhani kuwa ni kuokoa gharama ambapo mwisho wa siku hujikuta zimewagharimu pesa nyingi zaidi katika muda mrefu.
Kwa mfano, unaweza kuogopa kuajiri mhasibu na kuamua kutumia mtu ambae unamuona kuwa anauelewa kidogo ukidhani unaokoa gharama, mwisho wa siku unajikuta umeingia hasara zaidi ya ile hela ambayo ungemulipa muhasibu wa kukusaidia kila siku katika biashara zako.
ZINGATIA: Ingia gharama upate matokeo mazuri zaidi, Kutumia zaidi kidogo kuboresha ubora kazi zako.
Tunapofanya shughuli zetu za biashara ni vema tukawa makini ili kukuza kile tulichonacho, usikubali kuyumbishwa, fanya biashara kwa njia za kisasa zaidi hata kama biashara yako bado haijakua, Kwa wewe mwenye biashara yako naamini utakua umepata japo machache ya kuweza kukusaidia kutimiza ndoto zako za kibiashara.
Nipende kutoa shukrani zangu kwako wewe unaetumia muda wako kujifunza zaidi ili kutimiza ndoto zako zaidi.
No comments:
Post a Comment