Tatizo la nguvu za kiume ni tatizo linalowasumbua wanaume wengi kwa sasa;
Kwa bahati nzuri madaktari na watafiti mbalimbali wameendelea kufanya utafiti juu ya suluhisho la tatizo hili kwa njia salama zisizo na madhara mengine baadaye.
Tikiti maji ni tunda ambalo lina faida nyingi sana katika mwili. Kwanza, tunda hili huwa na virutubisho kama vile potasium, calcium, magnesium, carotene. Vitamini zingine ni kama vile vitamini A, B6, na C.
Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni ‘lycopene’, ‘beta-carotene’ na ‘citrulline’ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.
Tikiti maji ni viagra ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.
Kwenye tikiti maji hasa mbegu zake kuna kitu kingine kinaitwa ‘L-arginine’ ndicho ambacho huhusika na kuongeza nguvu za kiume. Mbegu za tikiti maji zimeonyesha matokeo mazuri katika kuimarisha nguvu za kiume hata kwa wazee kabisa.
Unachohitaji ni kula tikiti maji kila siku sambamba na mbegu zake na hutakawia kuona tofauti.
Faida nyingine 27 za tikiti maji kiafya
- Asilimia 92 yake ni maji
- Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
- Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili
- Huponya majeraha
- Hukinga uharibifu wa seli
- Huboresha afya ya meno na fizi
- Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
- Hubadilisha protini kuwa nishati
- Chanzo cha madini ya potasiamu
- Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la juu la damu
- Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
- Huondoa sumu mwilini
- Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake
- Husafisha figo
- Huzuia na kutibu kansa mbalimbali
- Tunda zuri kwa mwenye ugonjwa wa moyo
- Huzuia na kutibu pumu
- Hutibu tatizo la kufunga choo
- Hufanya ngozi ing’ae
- Huhamasisha kuota nywele
- Husaidia kupunguza uzito
- Huimarisha mifupa
- Husaidia kuponya vidonda na majeraha
- Huzuia madhara yasitokee katika seli
- Huzuia ugonjwa wa baridi yabisi ya moyo (heart stroke)
Tujitaidi kutumia vitu vya asili kama matunda na kuachana na madawa mengine tunayoletewa ambayo si salama kwa afya zetu.
No comments:
Post a Comment