Kutoka shafiinad.com
mfano vifaranga vya kuku
Hakikisha banda la vifaranga pamoja na vyombo umepuliza dawa ya kuua bakteria kwa kutumia dawa ya VRID nk kabla hujaingiza vifaranga. pia Hakikisha unavifaa vya joto kama
(a) kama unatumia umeme au solar tumia Balbu, heater, modules nk.
(b) kama umeme huna tumia chemli, karabai, jiko la mkaa, vidumu vya maji ya moto, vyungu vya joto.
then Baada ya hapo kuanzia siku ya 1-5 wape Grucose(glocovent ya ndege) + Otc plus/chicken plus + vitamin either ununue Multivitamin/vitalstress au ununue molasses ya unga 1kg +40 litre za maji wape kila siku ni nzur. baada ya hapo Wakitimiza siku ya 7 wape chanjo ya Newcastle deases(mdondo) then uendelee kuwapa maji ya molasses baada ya kutoa maji ya mdondo masaa 2 yakipita.
wakitimiza wiki 2 yaan siku 14 zikiisha wape chanjo ya gomboro(uendelee na maji ya molases. mpaka hapo wakitimiza wiki 3 utarudia chanjo ya mdondo na kuwapa antibiotics kama Otc 20% au otc 50% +Amprolium kwa muda wa siku 4-8 na utaendelea na maji ya molases.
Wakitimiza wiki ya wape chanjo ya Ndui(fowlpox) pamoja na dawa ya minyoo kama Ascaress( piperazine)
NOTE chanjo zote utarudia kila baada ya miezi 3.
Chakula cha vifaranga kuanzia siku ya 1 mpaka wiki ya 8 wape either sterter / chick mash na kuanzia miezi 3-4 wape Chakula aina Growers /finisher nk.
Wakifisha miezi 5 nashaur anza kuwapa Chakula aina ya Layers mash 50 kg +1 kg ya G.L.P so G.L.P ni aina ya virutubisho vyenye kuongeza wingi wa utagaji wa mayai kwa ndege.
wakifikisha wiki ya 16 kata midomo kisha wape Neoxyvital mfululizo kwa muda wa siku 4-6. hakikisha usafi wa banda na vyimbo ndo nguzo ya msingi hakikisha kila baada ya miezi 3 unapuliza dawa kuuwa bakteria kama VRID pia zingatia muda sahihi wa madawa kwa magonjwa yote ya kuku iwe ya Virus, Bakteria nk pia maji safi ni muhimu kitaalamu kuku mmoja hunywa maji robo litre na gram 125/150 za chakula per day so ukizingatia hvyo hakika utaona mafanikio ya ufugaji acha kufuga fuga kibiashara…
No comments:
Post a Comment