KANUNI KUU TANO ZA MAFANIKIO KIUCHUMI - MAARIFA

Breaking

Karibu katika blog ya mariffa kuweza kutambua Ujasiliamali na kujikwamua kiuchumi ahsante

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 30 May 2017

KANUNI KUU TANO ZA MAFANIKIO KIUCHUMI

Habari za leo ndugu,
Nisiku nyingine tena ambayo Mungu ametuwezesha kuiona, ni vema kumshukuru Mungu kwa hilo maana ni wengi walitamiani kuiona siku ya leo lakini hawakuweza.
Ni wakaribishe kwa siku ya leo kushirikiane  kujifunza  kanuni hizi Tano (5) za mafanikio kiuchumi ambazo naamini tukizifanyia kazi zinaweza kutusaidia katika kutimiza ndoto zetu;
1.      Jifunze kuweka akiba ya kipato chako:
v Ni kweli kwamba kipato chetu kinapoongezeka hata mahitaji pia huwa yanaongezeka; lakini ni vema tukajitaidi kulingana na kipato hicho hicho kidogo  angalau tubaki na akiba.
Ni vizuri sana kujiwekea akiba lakini pia ni vizuri zaidi kuweka akiba yenye malengo, tofauti ha hapo utajikuta unaitumia akiba hiyo kwa vitu visivyo na manufaa.
Tunaposema akiba wengi huwa tunachanganya tukiamini kuwa akiba ni kile kinachobakia baada ya matumizi yote, “hapanaa” Akiba ni kile kiasi kinachotengwa kabla ya matumizi. Kwa mfano  umeingiza kiasi  50,000 hakikisha  unatemga hata 20% kwa ajili ya kujiwekea  akiba  kulingana na kiasi ulichopata kwa siku au mwezi huo.
Kwa kufanya hivyo naamini matokeo utayaona.
2.      Usiwe mtu wa madeni (Kuendekeza madeni).
v  Kwanini nakwambia “Usiwe mtu wa Madeni”; deni ni Ugonjwa unaoweza kukutoa uhai wako wakati wowote na saa yoyote. Tumeshuhudia wengi wakijiua/Mali zao kuuzwa kwa sababu ya kuwa na madeni mengi.
Hata siku moja hutaweze kuwa na maendeleo kama ni mtu wa madeni, utakuwa mtu wa kuhamisha madeni na itakufanya kuwa mtuwa.
Usinielewe tofauti, sijasema usikope namaanisha usiyaendekeze yakawa sehemu ya Maisha yako. Kopa kwa malengo na pia ukiwa na uhakika wa kulipa deni hilo.
Ø  N.B. Usikope zaidi ya nusu ya kipato chako au mshahara wako maana hutaweza kuulipa utakufanya uwe mtumwa.
3.      Iheshimu na kuithamini pesa iliyoko mikononi mwako leo.
v  Katika jamii zetu tumekua na watu ambao ni matajiri sana na wenye uwezo lakini siri yao kubwa ni kutoidharau pesa, wapo wengi wanakwambia “siwezi kuokota 200/= hee!” mi mwenzako nikiiona naichukua maana naamini 200/= hiyo inaweza kunisaidia kupata huduma nitakayoihitaji hata kama ni ndogo.
v  Pesa unapoitumia vibaya siku zote utaiona ikipita mikononi mwako na hautaifanyia kitu chochote cha maana. tukiangalia matajiri wengi wanaotuzunguka hawayumbi kiuchumi kwa sababu wanaijua pesa lakini hawana mazoea na pesa.
v  Hata kama mfukoni au kenye account yako ya benk una mabilioni ya pesa, jitaidi uwezavyo kuiheshimu na kuithamini mia moja iliyoko mkononi mwako.
Ø  N.B. Ebu tujifunze zaidi  kuijua pesa na si kuizoea pesa na kuidharau.
4.      Kuwa na marafiki wanaokupa changamoto au wenye ndoto za kufanikiwa.
v  Nimejifunza sana katika hili, Ule usemi unaosema “niambie rafiki yako nikwambie tabia yako”; Huu usemi kila siku unanipa changamoto sana kwamba ile jamii na mazingira yanayo kuzunguka yanaweza kuwa mchango mkubwa kwa wewe kutokufikia ndoto zako au mafanikio unayoyahitaji, kwa mfano niambie kuhusu yule mtu ambaye mazingira yanayomzunguka wengi ni walevi wa kupindukia, wavuta bangi, au marafiki walio ulio nao vipi wanandoto za kufika mbali? au ni wale ambao wameshaandaliwa kila kitu na wazazi wao? Vipi maongezi yenu huwa yanahusu nini zaidi?  Kuna unachojifunza chochote kulingana na maongezi yenu ya kila siku?
v  Uhusiano mzuri na wale watu wanaotuzunguka pia utatufanya tuweze kufikia mafanikio kupitia frusa tutakazozipata ndani ya jamii zetu; hivyo basi  nivema tukaangalia marafiki tulionao na mchango wao katika mafanikio na katika kusaidiana ili kutimiza ndoto zetu.
5.      Kuwa mtu wa kujifunza kila wakati.
v  Wakati tunapambana na kutaka kutimiza ndoto zetu za kufanikiwa kiuchumi, tunatakiwa kuwa watu wa kujifunza; kama ni mwajiriwa tumia muda ulionao kupata ujuzi wa ziada kulingana na kazi uliyo nayo, kama ni mfanya biashara ongeza juhudi kuijua zaidi biashara, jifunze zaidi kuyajua mambo yako binafsi. Kama ni kazini kwako ebu angalia ni kitu gani kimepungua na endapo utakijua zaidi kinaweza kukuongezea manufaa kazika kazi zako.
v  Mwingine atapenda kujua ni jinsi gani ataongeza ujuzi?; dunia ya sasa iko mikononi naamini kwa kutumia simu  au computer yako kwa kuingia mtandaoni hutatoka kama ulivyoingia, soma habari za maana achana na habari za udaku ambazo zitakupotezea muda wako.
v  Tumia muda wako kwa kusoma vitabu, kuhudhuria tamasha au semina za biashara, ujasiriamali naamini kwa kufanya hivyo utaweza kuzitimiza ndoto zako za kufanikiwa kiuchumi.
Kwa kumalizia nipende kutoa tahadhari kwako wewe na mimi ambao tunazo ndoto za kufanikiwa, katika hii safari tunakutana na changamoto nyingi sana, wapo watakao kukatisha tamaa kuwa hutaweza, utatengwa na jamii hata ndugu pia kwa kukataa kile wanachokiamini wao na kukishikilia kile unachokiamini. Naamini kwa kila tunachokifanya tukimutanguliza Mwenyezi Mungu tutafanikiwa.
Kwa leo niishie hapa, nikuombe wewe rafiki, ndugu na jamaa ambae umeamua kupambana ili kuifikia ndoto ya mafanikio uendelee kufuatilia ukurasa huu ili tuendelea kufundishana na kusaidiana kadri Mwenyezi Mungu atakavyozidi kutubariki.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here