
Ndugu,Swala la mahusiano limekua ni tatizo sana
katika jamii zetu, limekua ni chanzo cha migongano ndani ya jamii, watu kuuana,
wengine kujiua, na hata kupelekea walio kwenye ndoa zao kuzikimbia na kusababisha ongezeko la watoto mitaani
wasio na walezi.
Zifuatazo ni Tabia zitakazoweza kuongeza
furaha na kufanya mahusiano yenu au ndoa yenu idumu;
Inaleta mvuto pale familia inapokaa pamoja kwa ajili ya kupata chakula hasa chakula cha jioni, watu wengi huwa wanaona jambo hili kuwa halina maana yoyote, leo naomba nikwambie ndugu yangu, kuna nguvu kubwa ya upendo na furaha pale munapokaa pamoja na kupata chakula kama familia.
Hii haina maana ya kwenda
kufanya ngono kila usiku, bali kwenda kulala kwa wakati mmoja.
Wanandoa
wanakumbushwa kwamba " wanatakiwa kupinga jaribu la kwenda kulala
kwa nyakati tofauti" hata kama mtu anabaki
nyuma isiwe kwa muda mrefu.
Pale wanandoa wanapoenda
kulala kwa pamoja kwa muda waliojiwekea, inaongeza furaha na amani.
- Daima kuaminiana na
kujaribu kusamehe
Ni wazi hii inategemea na
kiwango cha kutokubaliana, lakini nivema mahusiano yenu yakawa ya uaminifu,
mwamini mwenzako. Pia tambua hakuna binadamu aliyekamilia, amini kuwa mwenzako
amekosea kwa kutokujua na siyo kwa makusudi, mahusiano yenu yaruhusu msamaha na
si vinginevyo.
- Sema
"Nakupenda" na "kuwa na siku njema"
kila asubuhi mwambie mwenza
wako au mpenzi wako kumtakia majukumu mema. itamfanya ajisikie vizuri na
kuendelea kuiona thamani yako na kuona kuwa unamjali na kumthamini.
Tafuteni muda wa kuwa
pamoja na mwenza wako bila watoto, hii itawafanya kukumbuka mwanzo wa maisha ya mahusiano yenu kabla ya
kuwa na watoto na kufanya upendo wenu uongezeke na kutathimini wapi mumetokea
hadi kufikia wakati huo.
wakati mwingine munapaswa
kufanya shughuli ya pamoja, si tu kuangalia televisheni.
Dk Goulston anatuhimiza
kukumbatiana na wapenzi wetu kila
siku (kama hali inaruhusu). "Ngozi
yetu ina kumbukumbu ya 'kugusa nzuri',
unapomsalimia mwenzako kwa
kumkumbatia kuna mfanya ajisikie kupendwa na kuthaminiwa zaidi.
Wakati mwingine munatakiwa
kushikana mikono mukiwa munatembea pamoja. Ni ishara ya umma ya upendo,
Dr. Goulston anashauri
kwamba kushikana mikono na mwenza wako ni
ishara ya faraja ya kweli.
- Mtakie usiku mwema mwenza
wako kila usiku.
Bila kujali jinsi
unavyohisi. Kwa mujibu wa Dk Goulston anasema, hata ishara ya kusema usiku
mwema "inamwelezea mpenzi wako kwamba, bila kujali hali uliyonayo au matatizo yaliyopo au
migongano inayojitokeza.
Nimalizie kwa kukushukuru kwa kukubali kutumia muda wako kujifunza na kutaka kujua zaidi juu
ya mahusino.
Karibu tuendele kujifunza
pamoja.
No comments:
Post a Comment